top of page

Majina ya dawa ya kibiashara

Sefal ni dawa gani?

Sefal 25

Sefal 25 ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama Cinnarizine, inayotumika katika matibabu ya homa ya mwendo yenye dalili za kizungungu, kichefuchefu na kutapika na magonjwa mengine yatokanayo na madhaifu ya ndani ya sikio.

Levoz ni dawa gani?

Levoz 500

Levoz 500 ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama levofloxacin, aina ya antibayotiki katika kundi la quinolone inayotumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.

Gludown  ni dawa gani?

Gludown 500

Gludown 500 ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama metformin, moja ya dawa katika kundi la biguanide inayotumika kutibu kisukari aina ya 2.

Omesk ni dawa gani?

Omesk

Omesk ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama Omeprazole, aina ya dawa katika kundi la vizuia pampu ya protoni inayotumika kutibu magonjwa yanayotokana na uzalishaji mkali wa tindikali tumboni na kucheua tindikali.

Claranta 500 ni dawa gani?

Claranta 500

Claranta 500 ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama clarithromycin, aina ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.

Biazin XL ni dawa gani?

Biaxin XL

Biaxin XL ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama clarithromycin, aina ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii.

bottom of page