top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

Dkt. Mangwella S, MD

3 Novemba 2026, 15:48:56

Ini kusinyaa na kuwa na makovu (cirrhosis)

Ini kusinyaa na kuwa na makovu (cirrhosis)

Majina mengine: inivipele; liver cirrhosis (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: makovu ya kudumu (fibrosis) na vinundu kwenye ini.


Maelezo zaidi


  • Dalili: uchovu, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, manjano, tumbo kujaa maji (asaitizi), miguu kuvimba, kutokwa na damu kirahisi, kutapika damu, kuchanganyikiwa.

  • Visababishi: homa ya ini B na C, pombe, mafuta kwenye ini (unene, kisukari), kichocho, baadhi ya dawa na magonjwa ya kinga.

  • Makovu hayapotei, lakini kuacha pombe na kutibu homa ya ini huzuia ugonjwa kuendelea; huongeza hatari ya saratani ya ini.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kutapika damu, kinyesi cheusi, kuchanganyikiwa au kusinzia sana, homa na tumbo kuuma kwa mwenye ugonjwa wa ini – ni dharura.


Tazama pia: Homa ya ini (hepatitis)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page