top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

15 Novemba 2026, 07:51:30

Homa ya ini (hepatitis)

Homa ya ini (hepatitis)

Majina mengine: homa ya kirusini; homaini; hepatitis (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: uvimbekinga wa tishu za ini.


Maelezo zaidi


  • Hepatitis A na E: huambukizwa kwa chakula/maji machafu; mara nyingi hupona.

  • Hepatitis B, C, D: huambukizwa kwa damu, kujamiana na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto; zinaweza kuwa sugu na kuleta ini kusinyaa (cirrhosis) na saratani ya ini.

  • Dalili: uchovu, kichefuchefu, maumivu chini ya mbavu za kulia, manjano, mkojo mweusi – lakini wengi wenye aina sugu hawana dalili.

  • Kuzuia: chanjo ya homa ya ini B (watoto wachanga na watu wazima walio hatarini), usalama wa damu na sindano, kondomu, usafi wa chakula na maji.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Manjano, kuchanganyikiwa, kutokwa na damu, tumbo kujaa maji; au kupima homa ya ini B kama hujawahi kupima.


Tazama pia: Uvimbekinga mkali wa ini (acute hepatitis); Virusi vya homa ya ini (hepatitis viruses)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page