top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Kuharisha (diarrhoea)

Kuharisha (diarrhoea)

Majina mengine: kuhara; diarrhoea (Kiingereza)


Aina ya neno: dalili


Maana: kinyesi cha maji au laini, mara nyingi kuliko kawaida.


Maelezo zaidi


  • Aina: ya ghafla (chini ya wiki 2 – mara nyingi virusi, bakteria au chakula/maji machafu), ya muda mrefu (zaidi ya wiki 2), na yenye damu (kuhara damu – dysentery).

  • Huduma muhimu: ORS na maji mengi; kwa watoto, ORS pamoja na zinki kwa siku 10–14 na kuendelea kunyonyesha na kula.

  • Kuzuia: maji safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni, usafi wa chakula, vyoo bora, chanjo ya rotavirus.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Damu kwenye kinyesi, homa kali, kutapika kila kitu, macho kuzama, kukojoa kidogo, mtoto kusinzia sana au kukataa kunyonya, au kuharisha zaidi ya siku 3.


Tazama pia: Dawa zisizohitaji cheti (OTC)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page