top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Kumeza kwa shida (disifeijia)

Kumeza kwa shida (disifeijia)

Majina mengine: disfagia; dysphagia (Kiingereza)


Aina ya neno: dalili


Maana: ugumu wa kupitisha chakula kutoka mdomoni hadi tumboni.


Maelezo zaidi


  • Ya koo: kukohoa au kukabwa wakati wa kumeza, chakula kurudi puani – mara nyingi baada ya kiharusi au magonjwa ya neva.

  • Ya umio: chakula kukwama kifuani – mf. kubanwa kwa umio, akalazia, saratani ya umio, vidonda vya asidi.

  • Kumeza kwa maumivu huitwa odinofeijia (odynophagia).


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kumeza kwa shida kunakoongezeka, hasa vyakula vigumu kwanza kisha vya maji, pamoja na kupungua uzito – ni lazima kuchunguzwa haraka (saratani ya umio).


Tazama pia: Akalazia (achalasia)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page