top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Kuotesha vimelea na kupima usugu (culture and sensitivity)

Kuotesha vimelea na kupima usugu (culture and sensitivity)

Majina mengine: kipimo cha usikivu wa bakteria kwenye dawa; culture and sensitivity, C/S (Kiingereza)


Aina ya neno: kipimo cha maabara


Maana: sampuli (mkojo, damu, usaha, makohozi n.k.) huoteshwa ili vimelea vikue, kisha hupimwa dhidi ya antibiotiki mbalimbali.


Maelezo zaidi


  • Matokeo huonyesha kimelea na kama ni sikivu (dawa inafanya kazi) au sugu (dawa haifanyi kazi) kwa kila dawa.

  • Majibu huchukua siku 2–3 au zaidi.

  • Ni bora kuchukua sampuli kabla ya kuanza antibiotiki.


Tazama pia: Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page