top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Kushindwa kutunza kumbukumbu mpya (anterograde amnesia)
Majina mengine: kumbusasa iliyoathirika; kutotunza kumbukumbu mpya; anterograde amnesia (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: kushindwa kuunda kumbukumbu mpya baada ya tukio lililoathiri ubongo.
Maelezo zaidi
Mtu anaweza kuuliza swali lilelile mara kwa mara au kusahau alichofanya dakika chache zilizopita.
Visababishi: majeraha ya kichwa, upungufu wa vitamini B1 (Wernicke–Korsakoff), maambukizi ya ubongo, baadhi ya dawa, kiharusi.
Kinyume chake ni retrograde amnesia – kusahau mambo ya kabla ya tukio.
Tazama pia: Kupoteza kumbukumbu (amnizia)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

