Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Kupoteza kumbukumbu (amnizia)
Majina mengine: amnizia; amnezia; amnesia (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: upotevu wa kumbukumbu za zamani au kushindwa kutunza kumbukumbu mpya.
Maelezo zaidi
Aina kuu: kushindwa kukumbuka matukio ya kabla ya tukio (retrograde – kumbuzama) na kushindwa kutunza kumbukumbu mpya baada ya tukio (anterograde – kumbusasa).
Visababishi: majeraha ya kichwa, kiharusi, maambukizi ya ubongo, degedege, upungufu wa vitamini B1 kwa watumiaji wa pombe, upungufu wa akili (dementia), dawa, msongo mkubwa wa kisaikolojia.
Kupoteza kumbukumbu baada ya jeraha la kichwa kunahitaji uchunguzi wa haraka.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Kupoteza kumbukumbu ghafla, baada ya jeraha la kichwa, au pamoja na kuchanganyikiwa, udhaifu au kuongea kwa shida.
Tazama pia: Kushindwa kutunza kumbukumbu mpya (anterograde amnesia); Amnizia ya kweli
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

