top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:28:16

Kuvuja damu baada ya kujifungua (PPH)

Kuvuja damu baada ya kujifungua (PPH)

Majina mengine: postpartum haemorrhage, PPH (Kiingereza)


Aina ya neno: hali ya dharura ya uzazi


Maana: kuvuja damu kupita kiasi baada ya mtoto kuzaliwa.


Maelezo zaidi


  • Visababishi (4 T): mfuko wa uzazi kushindwa kubana (sababu kuu), majeraha ya njia ya uzazi, mabaki ya kondo la nyuma, damu kushindwa kuganda.

  • Kinga: kujifungulia kituo cha afya; oksitosini hutolewa mara baada ya mtoto kuzaliwa; kufuatilia mama kwa saa 24.

  • Matibabu: kuchua mfuko wa uzazi, dawa za kubana mfuko wa uzazi, tranexamic acid, maji na damu, na upasuaji inapohitajika.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Damu nyingi baada ya kujifungua (kujaza pedi ndani ya dakika chache), kizunguzungu au kuzirai – ni dharura.


Tazama pia: Kuvuja damu nyingi (haemorrhage), Upungufu wa homoni za pituitari baada ya kujifungua (Sheehan's syndrome)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page