Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Maumivu ya wengu (splenic pain)
Majina mengine: maumivu ya bandama; splenic pain, left upper quadrant pain (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: maumivu yanayotoka kwenye wengu.
Maelezo zaidi
Visababishi: wengu kuvimba (malaria, selimundu, homa za virusi kama mononucleosis), wengu kupasuka baada ya ajali, sehemu ya wengu kukosa damu (infarct – hasa selimundu), jipu la wengu.
Maumivu ya bega la kushoto pamoja na maumivu ya tumbo baada ya ajali huashiria damu tumboni.
Maumivu ya eneo hili huweza pia kutoka kwenye tumbo, kongosho, figo ya kushoto au mbavu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maumivu makali ya ghafla upande wa juu kushoto, hasa baada ya ajali au kwa mwenye wengu mkubwa, pamoja na kizunguzungu au kuzirai – ni dharura.
Tazama pia: Wengu (spleen)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

