Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Wengu (spleen)
Majina mengine: bandama; spleen (Kiingereza)
Aina ya neno: sehemu ya mwili
Maana: kiungo cha mfumo wa limfu na damu.
Maelezo zaidi
Wengu kuvimba (splenomegaly): malaria (ya muda mrefu au kujirudia), kichocho, selimundu kwa watoto wadogo, saratani ya damu, homa ya matumbo, ini kusinyaa, VVU.
Wengu uliovimba huweza kupasuka kwa pigo dogo – wenye wengu mkubwa waepuke michezo ya kugongana.
Asiye na wengu (baada ya upasuaji au kuharibika kwa selimundu) yuko hatarini zaidi kwa maambukizi makali – apate chanjo maalum na kinga ya malaria.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maumivu ya tumbo upande wa juu kushoto baada ya ajali au kupigwa, hasa pamoja na kizunguzungu – ni dharura (wengu kupasuka).
Tazama pia: Maumivu ya wengu (splenic pain), Ugonjwa wa selimundu (sickle cell disease)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

