top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:12
Mkakamao wa misuli usio wa hiari (distonia)
Majina mengine: dystonia (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: mikazo ya misuli ya muda mrefu isiyo ya hiari.
Maelezo zaidi
Ghafla baada ya dawa: dawa za saikosisi (mf. haloperidol) au za kutapika (metoclopramide) – hasa kwa vijana; hutibiwa haraka kwa sindano ya dawa maalum (mf. biperiden au diphenhydramine).
Aina nyingine ni za kudumu (mf. shingo kupinda, mkono wa mwandishi).
Si kifafa – mtu huwa na fahamu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Shingo, macho au ulimi kukakamaa ghafla baada ya kuanza dawa, hasa kukiambatana na kupumua kwa shida.
Tazama pia: Dawa ya saikosisi (antipsychotic), Mijongeo ya polepole ya kujinyonganyonga (athetosisi)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

