Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Mzio mkali (anaphylaxis)
Majina mengine: anafailaksis; anafailaksia; anaphylaxis (Kiingereza)
Aina ya neno: hali ya dharura
Maana: mzio mkali unaohusisha njia ya hewa, upumuaji au mzunguko wa damu.
Maelezo zaidi
Visababishi vya kawaida: dawa (penicillin, baadhi ya dawa za maumivu), vyakula (karanga, samaki, mayai), kuumwa na nyuki/manyigu, na latex.
Dalili: vipele na muwasho, kuvimba kwa uso, midomo au koo, kupumua kwa shida au wheeze, kizunguzungu au kuzirai, kutapika.
Tiba ya kwanza ni sindano ya adrenaline kwenye msuli wa paja, ikifuatiwa na huduma hospitali.
Aliyewahi kupata mzio mkali aepuke kichocheo na awaambie wataalamu wote wa afya.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Ni dharura ya mara moja – piga simu ya dharura au nenda hospitali sasa hivi.
Tazama pia: Mzio wa dawa
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

