top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:28:16

Nta ya sikio (cerumen)

Nta ya sikio (cerumen)

Majina mengine: earwax, cerumen (Kiingereza)


Aina ya neno: ute wa mwili


Maana: mchanganyiko wa mafuta, ngozi iliyokufa na ute wa tezi za sikio.


Maelezo zaidi


  • Sikio hujisafisha lenyewe – usichokonoe.

  • Nta iliyoziba hulainishwa kwa matone (mf. ya mafuta au ya kulainisha nta) kisha kuoshwa na mtaalamu.

  • Usisafishe sikio kwa maji ikiwa umewahi kuwa na tundu kwenye kiwambo cha sikio.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kupungua kwa kusikia, maumivu, majimaji kutoka sikioni au kizunguzungu.


Tazama pia: Mfereji wa nje wa sikio (external auditory canal)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page