top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

15 Novemba 2026, 04:34:20

Pepopunda ya kichanga (neonatal tetanus)

Pepopunda ya kichanga (neonatal tetanus)

Maana: Pepopunda katika siku 28 za mwanzo za maisha, inayotokana na sumu ya bakteria wa pepopunda walioingia kupitia kitovu kisicho safi.


Majina mengine: pepopunda ya mtoto mchanga (jina la zamani); neonatal tetanus (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa / dharura


Maelezo zaidi


Dalili


  • Kushindwa kunyonya baada ya siku chache za kunyonya vizuri.

  • Taya kufungwa.

  • Mwili kukakamaa.

  • Mishtuko inayochochewa na mguso au kelele.


Kinga


  • Chanjo ya pepopunda (TT/Td) kwa mama wakati wa ujauzito.

  • Kujifungulia kituo cha afya.

  • Kukata kitovu kwa kifaa safi.

  • Kutopaka chochote kwenye kitovu.


Ni ugonjwa unaotolewa taarifa kwa mamlaka za afya, na hutibiwa hospitali.


Lini umwone mtaalamu wa afya


Kichanga kinachoshindwa kunyonya ghafla au kukakamaa ni dharura; kipelekwe hospitali mara moja.


Tazama pia


Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page