top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer)

Saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer)

Majina mengine: cervical cancer (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa (saratani)


Maana: saratani ya seli za shingo ya kizazi (cervix).


Maelezo zaidi


  • Dalili (mara nyingi huanza baadaye): kutokwa na damu baada ya kujamiana, kati ya hedhi au baada ya kukoma hedhi; uchafu wenye harufu; maumivu ya nyonga.

  • Visababishi vya hatari: HPV, VVU, kuanza ngono mapema, wenzi wengi, sigara.

  • Kuzuia: chanjo ya HPV kwa wasichana, uchunguzi wa mara kwa mara (VIA au kipimo cha HPV) kwa wanawake wa miaka 25–49, na kutibu mabadiliko ya awali mapema.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kutokwa na damu isiyo ya kawaida ukeni, hasa baada ya kujamiana au baada ya kukoma hedhi.

  • Kila mwanamke: fanya uchunguzi wa shingo ya kizazi kama unavyoshauriwa (kila miaka 3–5).


Tazama pia: Saratani (cancer)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page