top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Saratani (cancer)

Saratani (cancer)

Majina mengine: kansa; uvimbe joto; uvimbejoto; cancer, malignancy (Kiingereza)


Aina ya neno: kundi la magonjwa


Maana: ukuaji usiodhibitiwa wa seli zisizo za kawaida (uvimbe wa saratani – malignant tumour).


Maelezo zaidi


  • Saratani za kawaida Tanzania: shingo ya kizazi, matiti, tezi dume, umio, ini, Kaposi sarcoma, saratani za damu.

  • Visababishi vya hatari: sigara, pombe, virusi (HPV, homa ya ini B na C, VVU), aflatoksini, unene uliokithiri, umri, historia ya familia.

  • Kuzuia na kugundua mapema: chanjo ya HPV na homa ya ini B, uchunguzi wa shingo ya kizazi na matiti, kuacha sigara.

  • Matibabu ni upasuaji, kemotherapia, tiba ya mionzi na tiba nyingine kulingana na aina na hatua.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Uvimbe usioisha, kidonda kisichopona, kutokwa na damu isiyo ya kawaida, kupungua uzito bila sababu, au kikohozi/sauti kukwaruza kwa zaidi ya wiki 3.


Tazama pia: Uvimbe usio wa saratani (benign tumour); Saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page