top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

15 Novemba 2026, 04:34:20

Sepsisi ya kichanga (neonatal sepsis)

Sepsisi ya kichanga (neonatal sepsis)

Maana: Maambukizi makali yaliyoenea mwilini na kwenye damu kwa kichanga, yaani mtoto mwenye umri chini ya siku 28.


Majina mengine: sepsisi ya mtoto mchanga (jina la zamani); neonatal sepsis (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa / dharura


Maelezo zaidi


Dalili


  • Kushindwa kunyonya.

  • Kulegea au kusogea tu anapoguswa.

  • Joto 37.5°C au zaidi, au chini ya 35.5°C.

  • Degedege.

  • Kupumua haraka au kifua kuvutwa ndani.

  • Manjano mapema.

  • Kitovu chekundu chenye usaha.


Vihatarishi


  • Chupa kupasuka mapema.

  • Homa ya mama wakati wa uchungu.

  • Kuzaliwa njiti au na uzito pungufu.

  • Kujifungulia nyumbani bila usafi.


Hutibiwa hospitali kwa dawa za kuua bakteria za sindano, kama ampicillin na gentamicin, pamoja na huduma ya joto na lishe.


Lini umwone mtaalamu wa afya


Kichanga chochote chenye dalili hizi kipelekwe hospitali mara moja, na kiendelee kunyonyeshwa njiani kama kinaweza.


Tazama pia


Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page