top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

6 Novemba 2026, 12:50:31

Shinikizo la damu linaloelekea kifafa cha mimba (Pri-eklampsia)

Shinikizo la damu linaloelekea kifafa cha mimba (Pri-eklampsia)

Majina mengine: shinikizo la kifafa cha mimba; Pri-eklampsia; pre-eclampsia (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa wa ujauzito


Maana: shinikizo la juu la damu la ujauzito pamoja na protini kwenye mkojo au viungo kuathirika.


Maelezo zaidi


  • Dalili za hatari: maumivu makali ya kichwa, kuona ukungu au mwanga unaomulika, maumivu ya tumbo la juu upande wa kulia, uso na mikono kuvimba ghafla, kukojoa kidogo, kupumua kwa shida.

  • Walio hatarini: mimba ya kwanza, mimba ya mapacha, waliowahi kupata kabla, shinikizo la juu la damu au kisukari kabla ya mimba, umri zaidi ya miaka 35, unene.

  • Kinga: wenye hatari kubwa hupewa aspirini dozi ndogo kuanzia wiki 12 na nyongeza ya kalsiamu kwa ushauri wa kliniki; kuhudhuria kliniki ya wajawazito na kupima shinikizo kila mara.

  • Matibabu: dawa za kushusha shinikizo, magnesium sulphate kuzuia degedege kwa hali kali, na kuzalisha mtoto kwa wakati unaofaa – tiba pekee ni kujifungua.

  • Huweza kutokea pia hadi wiki 6 baada ya kujifungua.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Mjamzito au aliyejifungua mwenye maumivu makali ya kichwa, kuona ukungu, maumivu ya tumbo la juu, uvimbe wa ghafla au degedege – nenda hospitali mara moja.


Tazama pia: Ujauzito (pregnancy), Kuvimba kwa kujaa maji (idima)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page