Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Trikomoniasisi (trichomoniasis)
Majina mengine: trikomonas; trichomoniasis (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa wa zinaa
Maana: maambukizi ya kimelea T. vaginalis kwenye uke au mrija wa mkojo.
Maelezo zaidi
Dalili kwa wanawake: uchafu wa ukeni mwingi wenye povu na harufu, kuwashwa na wekundu wa uke, maumivu ya kukojoa na wakati wa tendo la ndoa.
Kwa wanaume: mara nyingi hakuna dalili; wengine hupata kuwaka wakati wa kukojoa au uchafu kutoka kwenye uume.
Kwa wajawazito huongeza hatari ya kujifungua kabla ya wakati.
Matibabu: metronidazole kwa ushauri wa mtaalamu – wenzi wote wawili watibiwe pamoja; epuka pombe wakati wa dawa na saa 24–72 baadaye; tumia kondomu.
Pima VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Uchafu wa ukeni usio wa kawaida, kuwashwa, au maumivu ya kukojoa – nenda kituo cha afya.
Tazama pia: Kutokwa na ute ukeni (vaginal discharge), Metro (metronidazole)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

