top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

15 Novemba 2026, 07:51:30

Ugonjwa wa Meniere (Ménière's disease)

Ugonjwa wa Meniere (Ménière's disease)

Majina mengine: ugonjwa wa Ménière; Ménière's disease (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: kuongezeka kwa majimaji ndani ya labirinthi (endolymph) ya sikio la ndani.


Maelezo zaidi


  • Mara nyingi huanza sikio moja; kusikia hupungua zaidi kadri miaka inavyokwenda.

  • Mashambulizi huambatana na kichefuchefu na kutapika.

  • Huduma: kupunguza chumvi, kahawa na pombe; dawa za kizunguzungu wakati wa shambulio; dawa za kudhibiti kwa ushauri wa daktari wa masikio.

  • Hutofautiana na BPPV (vetigo ya sekunde chache ukibadili mkao) na uvimbekinga wa sikio la ndani (shambulio moja la siku kadhaa).


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kupungua kwa kusikia ghafla, au vetigo pamoja na kuona vitu viwili, kuongea kwa shida au udhaifu wa mwili – ni dharura.


Tazama pia: Kizunguzungu cha kuzunguka cha mkao (BPPV), Uvimbekinga wa sikio la ndani (labyrinthitis)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page