top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Ugonjwa wa selimundu (sickle cell disease)

Ugonjwa wa selimundu (sickle cell disease)

Majina mengine: selimundu; sikoseli; sickle cell disease, SCD (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa wa kurithi


Maana: kurithi jeni ya hemoglobini S kutoka kwa wazazi wote wawili (HbSS).


Maelezo zaidi


  • Mtoto hupata ugonjwa akirithi jeni kutoka kwa wazazi wote wawili; mwenye jeni moja ni mbebaji (sickle cell trait) – hana ugonjwa.

  • Dalili: upungufu wa damu, manjano, mikono na miguu kuvimba kwa watoto wadogo, maumivu makali ya mifupa, maambukizi, kukua polepole.

  • Huduma ya kudumu: kliniki ya selimundu, foliki asidi, penisilini ya kuzuia kwa watoto, chanjo zote, kinga ya malaria, hydroxyurea, maji mengi, kuepuka baridi na uchovu mkubwa.

  • Kipimo cha watoto wachanga na cha wapenzi kabla ya kuoana husaidia kupanga familia.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Homa 38.5°C au zaidi, maumivu makali yasiyopungua kwa dawa za nyumbani, kupumua kwa shida au maumivu ya kifua, weupe mkubwa, tumbo kuvimba ghafla, udhaifu wa upande mmoja, uume kusimama kwa maumivu muda mrefu – ni dharura.


Tazama pia: Hali kali ya ghafla ya selimundu (sickle cell crisis), Acute chest syndrome

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page