top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
15 Novemba 2026, 07:51:30
Utando wa moyo (perikadiamu)
Majina mengine: perikadiamu; pericardium (Kiingereza)
Aina ya neno: sehemu ya mwili
Maana: utando wa tabaka mbili – wa nje mgumu (fibrous) na wa ndani laini (serous) – unaozunguka moyo.
Maelezo zaidi
Uvimbekinga wake huitwa uvimbekinga wa utando wa moyo (pericarditis).
Maji au damu ikijaa ndani ya mfuko huu (pericardial effusion, haemopericardium) huweza kubana moyo.
Kutoa maji kwenye utando wa moyo kwa sindano (pericardiocentesis) hufanywa kwa uchunguzi au kuokoa maisha.
Tazama pia: Uvimbekinga wa utando wa moyo (pericarditis), Kipimo cha kuotesha majimaji ya perikadiamu
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

