Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
8 Novemba 2026, 11:56:45
Uvimbekinga wa utando wa moyo (pericarditis)
Majina mengine: perikadaitisi; pericarditis (Kiingereza); Uvimbe wa utando wa moyo
Aina ya neno: ugonjwa
Maana: uvimbekinga wa tabaka za utando wa moyo, mara nyingi pamoja na maji kujaa ndani yake.
Maelezo zaidi
Visababishi: virusi (kawaida duniani); Tanzania kifua kikuu ni chanzo kikuu, hasa kwa wenye VVU; figo kushindwa kufanya kazi (uraemia), magonjwa ya kinga, saratani, baada ya shambulio la moyo au upasuaji.
Daktari husikia sauti ya msuguano (pericardial friction rub); ECG na ultrasound ya moyo husaidia.
Maji mengi yakijaa haraka hubana moyo (cardiac tamponade) – dharura.
Matibabu kulingana na chanzo: dawa za kupunguza uvimbekinga (mf. ibuprofen, kolkisini), dawa za kifua kikuu, au kutoa maji kwa sindano.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maumivu ya kifua pamoja na kupumua kwa shida, kizunguzungu au kuzirai, mishipa ya shingo kuvimba au miguu kuvimba – ni dharura.
Tazama pia: Utando wa moyo (perikadiamu), Damu kujaa kwenye utando wa moyo (haemopericardium), Magonjwa ya moyo ya kuambukiza (infectious heart disease)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

