top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Uvimbe usio wa saratani (benign tumour)

Uvimbe usio wa saratani (benign tumour)

Majina mengine: uvimbe usio kansa; benign tumour (Kiingereza); uvimbe baridi


Aina ya neno: neno la magonjwa ya uvimbe


Maana: uvimbe ambao seli zake hazivamii tishu za jirani wala kusambaa (metastasis).


Maelezo zaidi


  • Mifano: uvimbe wa mafuta (lipoma), uvimbe wa mfuko wa uzazi (fibroids), uvimbe wa matiti (fibroadenoma).

  • Huweza kuondolewa kwa upasuaji ukiwa mkubwa, unaouma au unaobana.

  • Kinyume chake ni uvimbe wa saratani (malignant) unaovamia na kusambaa.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Uvimbe wowote unaokua haraka, mgumu, usiohamishika, unaouma, au unaotoa damu.


Tazama pia: Saratani (cancer)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page