Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
8 Novemba 2026, 11:56:45

Vipele vyenye maji (vesicular rash)
Majina mengine: harara lenge; vesicular rash, vesicles (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili / kiashiria cha ngozi
Maana: vipele vya majimaji vidogo (vesicles); vikubwa zaidi ya sm 0.5 huitwa malengelenge.
Maelezo zaidi
Tetekuwanga: vipele vingi mwili mzima, vya hatua tofauti kwa wakati mmoja, homa.
Mkanda wa jeshi: vipele vya upande mmoja vilivyopangika kwenye mstari, maumivu makali.
Malengelenge (herpes): kundi la vipele mdomoni au sehemu za siri.
Mkono-mguu-mdomo kwa watoto, uvimbekinga wa ngozi wa mguso, ukurutu, kuungua.
Usivipasue; viweke visafi; mwenye tetekuwanga akae mbali na wajawazito na watoto wachanga.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Vipele vya maji karibu na jicho, kwa mtoto mchanga, mjamzito au mwenye kinga dhaifu, au pamoja na homa kali, kupumua kwa shida au kuchanganyikiwa.
Tazama pia: Malengelenge (blisters), Mkanda wa jeshi (herpes zoster), Vipele (papules)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

