top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

i.m ni kirefu cha nini?

i.m katika tiba na dawa ni kifupisho cha neno ‘intramascular’ lenye maana ya ndani misuli.

Katika tiba au cheti cha dawa, endapo neno i.m litafuatiwa baada ya dawa humaanisha dawa hiyo itumike kwa kuchoma ndani ya misuli

i.v kirefu chake ni nini?

i.v kitiba hutumika kama kifupisho cha neno ‘intravenous’ lenye maana ya ‘ndani ya vena’. neno venous limetokana na neno la Kilatini ‘vena’

Kama dawa imeambatana na neno i.v inamaanisha dawa inatumika kwa kuchoma ndani ya mishipa ya vena

noct kirefu chake ni nini?

noct ni kifupi cha neno la Kilatini nocturnal lenye maana ya ‘usiku’

Katika tiba, endapo kifupisho hiki kimetumika kwenye cheti cha dawa au tiba hubaanisha dawa ‘itumike usiku’

o.d ni kirefu cha nini?

o.d katika tiba na cheti cha dawa ni kifupisho cha neno la Kilatini ‘omni die’ lenye maana ya ‘kila siku’ ingawa wataalamu wengi wa afya hutumia kifupisho o.d kumaanisha 'mara moja kwa siku' yaani dawa itumike mara moja kwa siku.

occul maana yake ni nini?

Occul hutumika katika tiba na cheti cha dawa kama kifupisho cha neno la Kilatini ‘occulent’ lenye maana ‘ya macho’

Dawa ikiandikwa na kufuatiwa na kifupisho occul humaanisha dawa hiyo inatumika kwa kutiwa machoni.

bottom of page