top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

tab ni kirefu cha nini?

Tab ni kifupi cha neno tablet chenye maana ya kidonge

tsp ni kirefu cha nini?

tsp katika tiba na dawa ni kifupisho cha neno 'teaspoon' lenye maana ya kijiko cha chai.

Kama kifupisho hiki kitatumika kwenye cheti cha dawa au matibabu ya mgonjwa humaanisha mgonjwa ‘atumie kipimo cha kijiko cha chai’.

ung ni kirefu cha nini?

ung katika tiba ni kifupisho cha neno la Kilatini ‘unguentum’ linalomaanisha dawa ya mafuta.

bottom of page