Growth hormone hufahamika kiswahili kama Homoni ya Ukuaji, ni homoni inayozalishwa na tezi ndogo ya pituitari na ambayo ina jukumu la msingi katika ukuaji wa mifupa, misuli, na tishu nyingine mwilini. Homoni hii pia inachangia udhibiti wa umetaboli wa mafuta, protini, na sukari.