Kamusi Tiba ya ULY CLINIC
Ballet’s sign
Ballet’s sign ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Ishara ya Ishara ya Ballet ambayo ni dalili ya kitabibu inayojitokeza pale ambapo misuli ya nje ya macho inayohusika na mjongeo wa macho hupooza au kudhoofika, hivyo mgonjwa hushindwa kusogeza macho juu, chini au pembeni kwa hiari licha ya mgonjwa kuwa na mjongeo wa hiari kwenye mwitikio wa mwanga katika mboni. Ishara hii ni kiashiria cha usumu wa thairoid.
Ballance’s sign
Ballance’s sign ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Ishara ya Ballance ambaypo ni dalili ya kitabibu inayopatikana katika majeraha ya wengu (Bandama), hasa pale kunapokuwa na kuvuja damu ndani ya tumbo (hemoperitoniamu). Dalili hii hudhihirika kwa kupatikana kwa ugumu usiobadilika upande wa kushoto wa tumbo kutokana na damu iliyoganda karibu na wengu, huku upande wa kulia wa tumbo ukionyesha ulaini unaobadilika kutokana na damu iliyo huru inayosogea kulingana na mkao wa mgonjwa.
Asynergy
Asynergy neno tiba lenye jina la kiswahili la "Asineji" ambapo ni hali ya kitabibu inayohusisha kushindwa kwa misuli au vikundi vya misuli kufanya kazi kwa mpangilio na uratibu unaotarajiwa wakati wa kutekeleza harakati fulani. Katika hali hii, sehemu za mwili ambazo kwa kawaida hufanya kazi kwa pamoja (kwa mfano bega, kiwiko na mkono) hushindwa kushirikiana ipasavyo, na kusababisha harakati zisizo kamilifu, zisizo laini, au zisizo na mfuatano sahihi. Asineji ni dalili ya uharibifu au usumbufu katika maeneo ya ubongo yanayosimamia uratibu wa mwendo.
Arroyo’s sign
Ishara ya Arroyo ni dalili ya kitabibu inayohusisha kuchelewa kwa kujikaza (kusinyaa) au kupanuka kwa mboni za macho (pupili) katika mwitikio wa mabadiliko ya mwanga. Katika hali hii, mboni haziitiki kwa haraka kama inavyotarajiwa, jambo linaloweza kusababisha hisia kali kwa mwanga (photophobia), hasa pale ambapo kujikaza kwa mboni kunachelewa.

Arthralgia
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Athraljia" ambayo ni hali ya kitabibu inayohusisha maumivu yanayotokea kwenye kiungo kimoja au zaidi bila kuwepo kwa uvimbe au dalili za wazi za uchochezi wa kiungo hicho. Hali hii huashiria kuwa kuna usumbufu au mkazo katika mfumo wa viungo, bila kuharibika moja kwa moja kwa muundo wa kiungo.
