top of page
Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Inflammation
Inflammation ni neno lenye jina la kiswahili la "Uchochezi wa kinga" au "Inflamesheni" ambapo ni mwitikio wa asili wa mfumo wa kinga ya mwili unaotokea baada ya jeraha, maambukizi au uharibifu wa tishu. Katika mchakato huu mishipa midogo ya damu hupanuka na kuruhusu damu, maji ya mwili, na seli za kinga kufika eneo lililoathirika.
bottom of page

