top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

17 Machi 2021 20:09:07

Ketoconazole na ujauzito

Ketoconazole na ujauzito

Ketoconazole ni yenye uwanja mkubwa wa kutibu fangasi aina mbalimbali, dawa hii imekuwa ikitumika bila kuleta mdhara kwa kichanga kwenye matibabu ya fangasi ukeni kwa mama mama mjamzito.Dawa hii ipo kundi sawa na watoto wa imidazole kama butoconazole, clotrimazole, econazole, miconazole,oxiconazole, sertaconazole,sulconazole, na tioconazole.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari (kwa dawa ya kunywa)

Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito (kwa dawa ua kupaka tu)


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari (kwa dawa ya kunywa)


NA


Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito (kwa dawa ua kupaka tu) ina maanisha nini?


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari (kwa dawa ya kunywa) ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu kwa matumizi kwa binadamu au taarifa chache zilizopo zinaonyesha kutohusiana na matatizo ya kiuumbaji kwa mtoto kama madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa hii inasababisha sumu kwa kwenye ukuaji wa kijusi cha wanyama jamii mbili waliopewa dawa hii kwenye dozi ambayo haisababishi sumu kwa mama mjamzito, dozi iliyo chini ya mara kumu ya dozi ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito (kwa dawa ua kupaka tu) ina maana gani?

Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, hata hivyo sifa ya ufanyaji kazi wa dawa inaonyesha kutokuwa na hatari yenye mashiko kusababisha madhara kwa kichanga aliye tumboni. Kwa mfano dawa zingine kwenye kundi moja au zenye kufanana ufanyaji kazi zinapatana na ujauzito au kiwango cha dozi ya dawa kwenye damu hakina mashiko kusababisha madhara. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Luscher KP, et al. Incidence of Candida infections during pregnancy and their treatment with ketoconazole ovula. Schweiz Rundsch Med Prax 1987;76:1285–7.

2. Product information. Nizoral. Janssen Pharmaceutics, 1997.

3. Nishikawa S, et al. Reproduction studies of KW-1414 in rats and rabbits. Clin Rep 1984;18:1433–88. As cited in Shepard TH. Catalog of Teratogenic Agents . 6th ed. Baltimore, MD: The Johns Hopkins University Press, 1989:1075.

4. Lind J. Limb malformations in a case of hydrops fetalis with ketoconazole use during pregnancy (abstract). Arch Gynecol 1985;237(Suppl):398.

5. Minkoff HL. Care of pregnant women infected with human immunodeficiency virus. JAMA 1987;258:2714–7.

6. Hobbs ER. Coccidioidomycosis. Dermatol Clin 1989;7:227–39.

7. Pont A, Williams PL, Loose DS, Feldman D, Reitz RE, Bochra C, Stevens DA. Ketoconazole blocks adrenal steroid synthesis. Ann Intern Med 1982;97:370–2.

8. Engelhardt D, et al. Ketoconazole inhibits cortisol secretion of an adrenal adenoma in vivo and in vitro. Klin Wochenschr 1983;61:373–5.

9. Divers MJ. Ketoconazole treatment of Cushing’s syndrome in pregnancy. Am J Obstet Gynecol 1990;163:1101.

10. Aron DC, et al. Cushing’s syndrome and pregnancy. Am J Obstet Gynecol 1990;162:244–52.

11. Amado JA, et al. Successful treatment with ketoconazole of Cushing’s syndrome in pregnancy. Postgrad Med J 1990;66:221–3.

12. Moretti ME, et al. Disposition of maternal ketoconazole in breast milk. Am J Obstet Gynecol 1995;173:1625–8.

13. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.

bottom of page