top of page

USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA  UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Aspirin kwa mjamzito

Aspirin kwa mjamzito

Matumizi ya aspirini wakati wa ujauzito haswa matumizi ya muda mrefu kwa dozi ndogo au matumizi ya mara moja moja katika dozi kubwa yanapaswa kuachwa. Dawa hii inaweza kudhuru hali ya ugandaji damu kwa mama na mtoto tumboni hivyo kuongeza hatari ya mtoto kufa, kutokuwa vema na ulemavu.

Sumatriptan kwa mjamzito

Sumatriptan kwa mjamzito

Sumatriptan licha ya kuwa na taarifa chache kutoka kwa watumiaji wakati wa ujauzito, ina hatari ya wastani kusababisha ulemavu kwa watoto wa wanyama waliopewa dawa hii kipindi cha ujauzito.

Diclofenac kwa mjamzito

Diclofenac kwa mjamzito

Tafiti zinaonyesha matumizi ya diclofenac katika kipindi cha 1 na cha 3 cha ujauzito huwa na hatari ya kupelekea madhaifu katika ujauzito na mtoto hivyo inashauriwa kutumia dawa zingine kipindi hiki.

Indomethacin kwa mjamzito

Indomethacin kwa mjamzito

Indomethacin imeonekana kuwa na hatari ya kusababisha ulemavu kwa kichanga kama itatumika kwenye kipindi cha kwanza na tatu cha ujauzito. Kuna taarifa chache kuhusu usalama wake wakati wa kunyonyesha hata hivyo inaweza patana na unyonyeshaji.

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Matumizi ya ciprofloxacin kipindi cha kwanza cha ujauzito huwa na uhusiano wa moja kwa moja wa kusababisha ulemavu kwa vichanga. Baadhi ya tafiti na wataalamu wa afya wanashauri kutotumia kabisa dawa hii wakati wa ujauzito.

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine hausababishi ulemavu kwa watoto wa wanyama wajawazito waliopewa dawa hii, hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha usalama wa dawa hii kwa binadamu.

Secnidazole kwa mjamzito

Secnidazole kwa mjamzito

Secnidazole ni dawa kundi la nitroimidazole iliyoruhusiwa kutumika mwaka 2017 na shirika la dawa la Amerika (FDA). Kuna taarifa chache zisizotosha kutoa jumuisho kuhusu usalama wake wakati wa ujauzito na kunyonyesha.

Stavudine na ujauzito

Stavudine na ujauzito

Stavudine ni dawa jamii ya NRTI inayotumika kutibu maambukizi ya VVU. Taarifa za wanyama na binadamu zinaonyesha kuwa stavudine inahatari kidogo ya kusaabisha ulemavu kwa kijusi na kichanga tumboni.

Ondansetron  na ujauzito

Ondansetron na ujauzito

Taarifa nyingi za wanyama na binadamu zinaonyesha kuwa dawa hii ina hatari kidogo ya kusababisha ulemavu kwa vichanga watakaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii.

Omeprazole na ujauzito

Omeprazole na ujauzito

Taarifa za tafiti zimeonyesha kuwa dawa jamii ya PPI ikiwa pamoja na Omeprazole zina hatari kidogo ya kusababisha ulemavu kwa vichanga ikitumika wakati wa ujauzito. Hata hivyo kuna kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi yake kwa binadamu wajawazito.

Lansoprazole na ujauzito

Lansoprazole na ujauzito

Taarifa za tafiti zimeonyesha kuwa dawa jamii ya PPI ikiwa pamoja na Lansoprazole zina hatari kidogo ya kusababisha ulemavu kwa vichanga ikitumika wakati wa ujauzito. Hata hivyo kuna kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi yake kwa binadamu wajawazito.

Amphetamine na ujauzito

Amphetamine na ujauzito

Ingawa matumizi ya amphetamine kama tiba huonekana kuwa na hatari kidogo kwa kichanga, matumizi yasiyo ya kitiba huwa sumu kali kwa kijusi na kichanga aliyezaliwa. Hivyo hairuhusiwi kutumika kwa matumizi yasiyo dawa kwenye ujauzito.

bottom of page