top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

19 Machi 2021 18:50:58

Rifabutin na ujauzito

Rifabutin na ujauzito

Hakuna taariza inayoelezea matumizi ya rifabutin kwa binadamu wajawazito, taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo na hatari kidogo ya kupata madhaifu ya kiuumbaji wa watoto wanaozaliwa na wanyama wajawazito waliotumia dawa hii. Hata hivyo, licha ya hatari hiyo kwa wanyama, faida za matumizi kwa binadamu ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza. Inapoanzishwa haitakiwi kuacha tumika kwa sababu ya ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo, ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa haileti sumu kwenye uumbaji wa kijusi (kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga

na


Haipatani na unyoyenyeshaji (kwa mgonjwa wa UKIMWI) ina maana gani?

Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga na Haipatani na unyoyenyeshaji (kwa mgonjwa wa UKIMWI) ina maana gani?


Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga ina maana gani?

Inaweza kuwa taarifa juu ya matumizi kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii hazipo au zipo chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Hairuhusiwi kumnyonyesha mtoto unapotumia dawa hii


Haipatani na unyoyenyeshaji (kwa mgonjwa wa UKIMWI) maana yake nini?

Kunawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha. Hata hivyo mkusanyiko wa taarifa zinaonyesha kuwa dawa huweza kuwa sumu kali kwa kichanga, au haishauriwi kunyonyesha endapo dawa itahitajika kutumika kwa mama mwenye anayehitajika kutumia dawa hii. Mama anatakiwa asinyonyeshe anapotumia dawa hii au akiwa na ugonjwa unaotakiwa kutumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Product information. Mycobutin. Pharmacia & Upjohn, 2004.

bottom of page