Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Rachel L, MD
Ijumaa, 5 Novemba 2021

Ulimi kuwaka moto
Ulimi kuwaka moto ni tatizo la ulimu kuwa na hisia za kuungua na wakati mwingine maumivu huwa makali kama vile umeungua na maji ya moto. Tatizo hili linaweza kuwa la kujirudia au limetokea kwa mara ya kwanza na huweza kuhusisha sehemu mbalimbali za kinywa kama ulimi, fizi, ndani ya mashavu, paa la mdomo na sakafu ya mdomo au mdomo wote.
Dalili
Dalili za ulimu kuwaka moto mbali na hisia za ulimi kuungua huweza kuwa pamoja na;
Kuhisi kinywa kimekuwa kikavu au kuwa na kiu sana
Kubadilika kwa randha ya chakula, kuhisi kama umekunywa dawa ya metronidazole, yenye radha ya metalik
Kupoteza hisia za radha ya chakula
Kuwashwa, kuchoma au kufa ganzi kwa ulimi
​
Visababishi
​
Vinaweza kuwa visababishi vya awali au visababishi vinavyotokana na Matatizo fulani mwilini;
Visababishi vya awali huwa mara zote haviambatani na mabadiliko ya kifiziolojia mwilini. Mtu akipimwa, kila kitu huonekana kipo sawa. Tafiti zinaonyesha maumivu haya huenda yakawa yanahusiana na mabadiliko kwenye mishipa ya fahamu.
​
Visababishi vingine huwa ni
​
Kinywa kikavu- husababishwa na magonjwa ya kushindwa kuzalisha mate, madawa aina fulani yanayozuia uzalishaji mate au matibabu ya saratani
Matatizo mengine ya kinywa- kama maambukizi ya fangas, michomo kwenye ngozi, au tatizo la ulimi ramani au kwa jina jingine ulimi jeografia
Upungufu wa viinirishi- Upungufu wa vitamin B12, madini ya zinc,vitamin B9, B1 B2 B6
Mzio/aleji- mzio na chakula aina fulani kama vitunza vyakula vya kusindikwa au vyakula vilivyoongezewa ladha isiyo halisi.
Tatizo la kucheua- tatizo la kucheua (GERD) husabaisha tindikali ya tumboni kuchoma ulimi na mtu kuhisi hali ya ulimi kuungua.
Madawa aina fulani- Madawa ya kushusha shinikizo la damu
Mazoea na tabia- tabia ya kutoa uliminje kwa nguvu, kujingata ulimiau, kung’ata meno huweza kuambatana na maatatizo ya ulimi kuwaka moto.
Matatizo ya homoni- kama ugonjwa wa kisukari, au upungufu wa homoni ya thyroid
Kuchokoza ulimi- kwa kupiga mswaki sana, kutumia dawa za meno zinazounguza, kutumia sana dawa zinazounguza ulimi kama zile za kusafisha ulimi, au kunywa vilevi vyenye tindikali kwa wingi.
Matatizo ya kisaikolojia- Mfano msongo wa mawazo, na huzuniko
Kuvaa meno bandia ambayo hayakai vema kwenye mdomo huweza kusababisha michomo kwenye ulimina kuhisi hali ya kuungua pia
Vihatarishi
​
Vihatarishi vya kupata tatizo hili la ulimi kuwaka moto ni
Hali ya kuwa na ugonwjwa hivi karibuni
Magonjwa sugu aina fulani kama ugonjwa wa parkinson’s, magonjwa ya shambulia la kinga za mwili na magonjwa ya mishipaya fahamu
Madawa aina fulani
Mzio na chakula au dawa aina fulani
Huzuniko
Kupata majeraha kwenye maisha
​
Mtu anaweza kupata madhara aina fulani akiwa na tatizo hili la ulimi kuwaka moto kama vile kushindwa kulala vema, kushindwa kula chakula, huzuniko na hofu iliyopitiliza.
Kujikinga
​
Hakuna njia ya kujikinga inayojulikana, mtu anaweza kuzuia baadhi ya vihatarishi mfano kuacha kuvuta sigara, kuacha vyakula vyenye tindikali na pilipili kwa wingi na vinywaji nyenye gesi ya carbon kama vile soda na kuepuka msongo wa mawazo.
​
Vipimo na matibabu
​
Vipimo vitahusisha kuchukuliwa historia ya tatizo lako na kuangaliwa ulimi. Daktari anaweza kuagiza vipimo mbalimbali ili kujua visababishi au madhara yaliyojitokeza au kuweza kujitokeza.
Tiba ya kuondoa tatizo kabisa bado haijulikani, hata hivyo tiba dhidi ya dalili zinazojitokeza zipo
​
Matibabu hayo yanahusisha
Kupata dawa za kurudisha mate kinywani
Dawa za kuosha kinywa
Dawa za kuondoa maumivu
Dawa za kutibu huzuniko au msongo wa mawazo
Matibabu ya kujitambua ili kuondoa hofu iliyopitiliza
​
Matibabu ya nyumbani
Kunywa maji ya kutosha, kuzuia tatizo la mdomo mkavu na unaweza kulamba barafu ya vipande vidogo vidogo
Zuia kula vyakula vyenye tindikali kwa wingi kama nyanya, juisi ya machungwa, ndimu na vinywaji vyenye gesi ya carbon mfano soda n.k
Acha kunywa pombe na vinywaji jamii ya pombe maana huamsha hisia za ulimi wako
Usivute sigara wala kutumia tumbaku
Jizuie kula vyakula vya moto vyenye viungo vingi
Usile vyakula vyenye mdalasini au kemikali ya minti kama pipi na baadhi ya dawa za meno
Tumia dawa za meno ambazo hazijawekewa radha
Chukua hatua kujikinga na msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi ya yoga, kushiriki michezo au kushirikiana na jamii, usikae mpweke