Magonjwa na saratani mbalimbali
Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Goita: Dalili, Visababishi, Vipimo na Matibabu
Ni kuongezeka kwa ukubwa wa tezi iliyopo mbele ya shingo (tezi thairoidi) kunakoweza kusababishwa na upungufu wa iodini, magonjwa ya kinga ya mwili, vinundu au matatizo ya homoni, hivyo uchunguzi wa mapema ni muhimu ili kubaini chanzo chake. Ingawa goita nyingi si hatari, uvimbe unaoongezeka, unaosababisha shida ya kupumua au kumeza, au unaoambatana na dalili nyingine zisizo za kawaida unapaswa kufanyiwa tathmini na mtaalamu wa afya ili kuzuia madhara na kuboresha matokeo ya matibabu.

Demataitisi ya Mguso
Demataitisi ya Mguso ni uvimbe wa ngozi unaotokea baada ya ngozi kugusana na kemikali au vitu vinavyoiudhi au kusababisha mzio, na huweza kuleta mwasho, wekundu, vipele na malengelenge. Kutambua na kuepuka kisababishi pamoja na kutumia matibabu sahihi husaidia kupunguza dalili na kuzuia tatizo kujirudia.

Kubanduka kwa ngozi
Kubanduka kwa ngozi ni dalili inayoweza kusababishwa na hali mbalimbali, kuanzia ukavu wa ngozi na kuungua na jua hadi maambukizi, magonjwa ya ngozi na athari za baadhi ya dawa. Kutambua chanzo cha tatizo mapema ni muhimu ili kupata matibabu sahihi na kuzuia madhara au kujirudia kwa dalili.

Kubanduka kwa ngozi ya viganja vya mikono
Hufahamika pia kama Keratolisisi eksifoliativa ,ni hali isiyo ya kuambukiza inayosababisha tabaka la juu la ngozi kubanduka mara kwa mara, hasa kwenye viganja na wakati mwingine nyayo za miguu. Ingawa si ugonjwa hatari, utambuzi sahihi na utunzaji mzuri wa ngozi husaidia kupunguza kujirudia kwa dalili na kutofautisha hali hii na magonjwa mengine ya ngozi yanayofanana.
