Mwandishi:
Dkt. Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
11 Novemba 2021 19:19:56
FEFO inafaida gani kwa mjamzito?
Ni dawa yenye virutubisho vya madini chuma na folic acid zilizo katika kundi la dawa zinazoongeza damu.
Mchanganyiko wa virutubisho hivi hutumika katika ujauzito ili kuzuia upungufu wa damu unaotokana na upungufu wa madini chuma pamoja na folic acid.
Faida za FEFO kwa mjamzito
Hupunguza hatari ya upungufu wa damu kutokana na ukosefu wa madini chuma na folic acid unaoweza kupelekea;
Kujifungua kabla ya mimba kukomaa
Kujifungua njiti
Kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua
Maambukizi kwenye uzazi wakati wa kujifungua
Folic acid hufanya kazi ya ziada kama vile
Kuzuia magonjwa kutokana na kasoro kwenye mfumo wa fahamu katika ubongo na uti wa mgongo kama vile mgongo wazi, ubongo kuumbwa chini ya kiwango na ubongo wazi. Soma zaidi kuhusu umuhimu wa folic acid kwa mjamzito katika maka nyingine ndnai ya tovuti hii.
Nini unapaswa kufahamu zaidi?
Pamoja na mama mjamzito kushauriwa atumie vidonge vya FEFO, unashauriwa kutumia vyakula pia vyenye virutubisho folic acid, madini chuma na vitamin C ambayo husaidia ufyonwaji wake,
Makala hii imejibu nini?
Makala hii imejibu maswali ya;
Faida za fefo kwa mjamzito
Fefo inatibu nini?
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
12 Novemba 2021 09:03:07
Rejea za mada hii
WHO.Folic acid and iron supplementantion. https://www.who.int/elena/titles/daily_iron_pregnancy/en/. Imechukuliwa 11.11.2021
Folic Acid & Neural Tube Defects: An Overview. CDC. https://www.cdc.gov/ncbddd/birthdefectscount/basics.html. Imechukuliwa 11.11.2021
CDC. Facts about Neural Tube Defects. https://www.cdc.gov/ncbddd/birthdefects/facts-about-neural-tube-defects.html. Imechukuliwa 11.11.2021