top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. David A, MD

20 Oktoba 2021 15:50:14

Kuna aina ngapi za mkojo wa mwanamke aliyekojozwa?

Kuna aina ngapi za mkojo wa mwanamke aliyekojozwa?

Tafiti inatambua aina moja tu ya mkojo unaotoka kwa mwanamke aliyekojozwa. Mkojo huo huwa na ujazo wa kijiko kimoja cha chai mweupe kama maziwa, wenye ladha tamu na hauna harufu ya mkojo.


Baadhi ya wanawake hata hivyo hutokwa na mkojo halisi wakati wa kufika kileleni kama kuna kiasi cha mkojo kilibakia kwenye mrija wa kutoa mkojo nje. Aina hii ya mkojo sio mkojo w akukojozwa bali ni mkojo wa kawaida tu.


Hisia na kutoa mkojo wa kukojozwa licha ya kutokea sana wakati wa mwanamke anapofika kileleni, huweza kutokea pia kabla ya muda huo. Wanawake wengi walioripoti kukojozwa, wameripoti kupata hisia kuu za raha ya kufanaya tendo tofauti na kufika kileleni kwa kawaida.


Kumbuka mwanamke anaweza kufika kileleni bila kukojozwa


Pata maelezo zaidi kuhusu mada ya maji ya kukojozwa sehemu nyingine katika tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Oktoba 2021 16:37:41

Rejea za mada hii

  1. Addiego, F., E. G. Belzer, J. Comolli, W. Moger, J. D. Perry, and B. Whipple. 1981. Female Ejaculation: A Case Study. The Journal of Sex Research, 17: 13– 21

  2. Belzer, E. G., B. Whipple, and W. Moger. 1984. On Female Ejaculation. The Journal of Sex Research, 20: 403– 406.

  3. Cabello, F. 1997. Female Ejaculation: Myths and Reality, pp. 1–8. In J. J. Borras-Vall and M. Perez-Conchillo, eds., Sexuality and Human Rights. Valencia: Nau Llibres.

  4. De Graff, R. 1672. New Treatise Concerning the Generative Organs of Women. Journal of Reproduction and Fertility, 17: 77– 232, edited by H. D. Jocelyn and B. P. Setchell. Oxford: Blackwell Scientific Publications, 1972.

  5. Perry, J. D., and B. Whipple. 1981. Pelvic Muscle Strength of Ejaculators: Evidence in Support of a New Theory of Orgasm. The Journal of Sex Research, 17: 22– 39.

  6. Sevely, J. L., and J. W. Bennett. 1978. Concerning Female Ejaculation and the Female Prostate. The Journal of Sex Research, 14: 1– 20.

bottom of page