top of page

Mwandishi:

Dkt. Lugonda B, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

23 Julai 2023 13:40:26

Maambukizi ya VVU kwa kushikana mikono

Unaweza kupata maambukizi ya VVU kwa kushikana mikono?

Je naweza kupata maambukizi ya UKIMWI kwa kushikana mikono na mwathirika? Hili ni moja ya swali ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza na kujibiwa katika makala hii.


Kirusi cha UKIMWI ama VVU au HIV mara nyingi huwa hakiambukizwi kwa shughuli za kila siku za nyumbani, shuleni au kwenye jamii kama vile kushikana mikono, kukumbatiana au kubusiana.


Je tafiti zinasemaje kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kusikana mikono?

Visa vichache vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI vimeripotiwa kuwa matokeo ya kushikana mikono ya mwathirika majumbani kwa kushika majimaji au damu ya mwathirika iliyotoka kwenye kidonda au jeraha.


Ingawa ugusaji wa majimaji na damu huweza kutokea sana majumbani, uambukizaji wa virusi vya UKIMWI kwa njia hii hutokea kwa nadra sana.

Hata hivyo, watu wenye maambukizi ya VVU na wahudumu wa wagonjwa wa VVU wanapaswa kupewa elimu ya kutosha na kufundishwa ipasavyo njia za kudhibiti maambukizi.


Wakat gani unaweza kupata maambukizi kwa kushikana mikono?

Unaweza kupata maambukizi kwa kushikana mikono endapo wewe una kidonda au jeraha kwenye mikono na chanzo cha VVU(mwathrika) kuwa na hali zifuatazo:

 • Kidonda au jeraha linalotoa damu au majimaji kwenye mikono

 • Vipele kwenye mikono vinavyotoa majimaji

 • Kuwa na virusi wengi kwenye damu kama kwa wasiotumia dawa na ana vipele vinavyotoa majimaji au damu

 • Kuwa na damu au majimaji kwenye mikono kutoka kwenye kidonda au jeraha lililo sehemu nyingine ya mwili

 • Kuwa na majimaji kwenye mikono kutoka kwenye maziwa, ute ukeni au kwenye uume au kwenye njia ya haja kubwa, shahawa na damu


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?

Unaweza kupata maelezo zaidi kwa kubofya makala zifuatazo:Majibu ya Makala hii

Makala hii imejibu maswali kuhusu

 • Unawez kaupata UKIMWI kwa kushikana mikono

 • Unaweza kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa kushikana mikono

 • Kushikana mikono kunaambukiza ukimwi

 • Wakati gani kushikana mikono huambukiza virusi vya UKIMWI?

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 13:40:26

Rejea za mada hii

 1. HIV. gov. How Do You Get or Transmit HIV?. https://www.hiv.gov/hiv-basics/overview/about-hiv-and-aids/how-is-hiv-transmitted/. Imechukuliwa 23.07.2023

 2. ULY CLINIC. Dawa king aya UKIMWI. https://www.ulyclinic.com/post/dawa-kinga-ya-ukimwi-ulyclinic. Imechukuliwa 23.07.2023

 3. ULY CLINIC. Virusi vya UKIMWI. https://www.ulyclinic.com/virusi/Virusi-vya-UKIMWI. Imechukuliwa 23.07.2023

 4. WHO. HIV and AIDS. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/hiv-aids#:. Imechukuliwa 23.07.2023

bottom of page