top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

12 Oktoba 2021 19:35:38

Nina mimba ya mwezi mmoja na nusu naweza tumia amlodipine kushusha presha?

Nina mimba ya mwezi mmoja na nusu naweza tumia amlodipine kushusha presha?

Ripoti ya tafiti tatu zilizohusisha jumla ya wanawake wajawazito watano zinaelezea miishio ya matumizi ya amlodipne kwa ujauzito kama ifuatavyo;


  • Watoto wawili kuzaliwa wakiwa hawana shida yoyote

  • Kichanga mmoja alizaliwa hajakuwa vema (inafikiriwa kutosababishwa na dawa kutokana na muda wa kuanza kutumia dawa)

  • Mtoto moja alikufa bila sababu kufahamika lakini inawezekana kuhusiana na dawa

  • Mtoto moja alizaliwa na ugonjwa nadra wa ngozi unaodhaniwa kuhusiana na dawa


Taarifa za tafiti nyingine zaidi zinaonyesha amlodipine kuzuia ukuaji wa mtoto tumboni ukifananisha na dawa zingine za kushusha shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito.


Kutokana na taarifa hizo na zingine zilizofanyika kwa wanyama, amlodipine inaonekana kuwa na taarifa chache kuhusu matumizi yake kwa binadamu wajawazito, licha ya taarifa za wanyama kuoneysha kuwa na hatari ya wastani ya kusababisha madaifu ya kiuumbaji kwa mtoto tumboni.


Inashauriwa siku zote kutumia dawa ambazo zina taarifa nyingi kuhusu usalama wake wakati wa ujauzito kuliko dawa ambazo zina taarifa chache. Tumia dawa salama zaidi kwa afya ya kichanga aliye tumboni.


Soma zaidi kwenye usalama wa amlodipine kipindi cha ujauzito na kunyonyesha kwenye makala za usalama wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Oktoba 2021 21:00:24

Rejea za mada hii

  1.  Product information. Norvasc. Pfizer, 2000.

  2. Rosbotham JL, et al. Painful subcutaneous fat necrosis of the newborn associated with intra-partum use of a calcium channel blocker. Clin Exp Dermatol 1998;23:19–21.

  3.  Ahn HK, et al. Exposure to amlodipine in the first trimester of pregnancy and during breastfeeding. Hypertens Pregnancy 2007;26:179–87.

  4. Nahapetian A, etal. Serial hemodynamics and complications of pregnancy in severe pulmonary arterial hypertension. Cardiology 2008;109:237–40.

  5. Malha, et al. “Safety of Antihypertensive Medications in Pregnancy: Living With Uncertainty.” Journal of the American Heart Association vol. 8,15 (2019): e013495. doi:10.1161/JAHA.119.013495.

bottom of page