top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L ,MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

21 Oktoba 2021 18:40:12

Penadur injection inatibu nini?

Penadur injection inatibu nini?

Penadur injection ni jina la kibiashara la ceftriaxone. Ceftriaxone injection ni dawa jamii ya cephalosporin kizazi cha tatu yenye wigo mpana wa kuua bakteria kwenye jamii ya gramu hasi na chanya. Dawa hii imehifadhiwa kutumika kwenye baadhi ya matibabu tu yanayosababishwa na bakteria na inaweza tumika yenyewe au au pamoja na dawa nyingine ili kuongeza wingo wa uuaji wa vimelea vya maradhi.


Penadur injection hutibu nini?


Penadur au Ceftriaxon injection inaweza tumika yenyewe au pamoja na dawa zingine kutibu magonjwa yafuatayo;


 • Magonjwa ya zinaa kama vile gono

 • Maambukizo kwenye via vya uzazi vya mwanamke (PID)

 • Homa ya uti wa mgongo

 • Maambukizi ya bakteria kwenye mapafu (nimonia)

 • Maambukizi kwenye masikio, ngozi, damu, mifupa, maungio ya mifupa

 • Maambukizi ya bakteria kwenye tumbo


Kazi zingine za penadur

Mbali na kutibu maradhi hayo, penadur injection hutumika kabla ya kufanyiwa upasuaji kuzuia maambukizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji.


Kumbuka

Watu wengi wamekuwa wakitumia ceftriaxone kwa kupewa na wataalamu au kujitibu wenyewe pasipo kuwa na uhaja wa dawa hiyo, hii imepelekea vimelea wa maradhi kuwa sugu kwenye dawa hii na kupungua kwa ufanisi wake wa matibabu.


Mfano watu wengi ikiwa pamoja na wataalamu wasio na weledi hutumia dawa hii ikiwa yenyewe kutibu gono au magonjwa mengine ya zinaa, hii si sahihi na wagonjwa wengi huwa hawaponi. Wasiliana na daktari kwani wana utaalamu wa kufahamu tatizo lako na ufahamu wa dawa gani utumie kulingana na dalili ulizonazo.


Rai


Epuka usugu wa vimelea wa maradhi kwenye dawa hii kwa kuitumia dawa baada ya kushauriwa na daktari tu.


ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

21 Oktoba 2021 18:57:13

Rejea za mada hii

 1. Richards DM, et al. Ceftriaxone. A review of its antibacterial activity, pharmacological properties and therapeutic use. Drugs. 1984 Jun;27(6):469-527. doi: 10.2165/00003495-198427060-00001.

 2. Park HZ, et al. Ceftriaxone-associated gallbladder sludge. Identification of calcium-ceftriaxone salt as a major component of gallbladder precipitate. Gastroenterology. 1991 Jun;100(6):1665-70. doi: 10.1016/0016-5085(91)90667-a.

 3. Lee S, et al. Pharmacokinetics of a new, orally available ceftriaxone formulation in physical complexation with a cationic analogue of bile acid in rats. Antimicrob Agents Chemother. 2006 May;50(5):1869-71. doi: 10.1128/AAC.50.5.1869-1871.2006.

 4. Garot D, et al. Population pharmacokinetics of ceftriaxone in critically ill septic patients: a reappraisal. Br J Clin Pharmacol. 2011 Nov;72(5):758-67. doi: 10.1111/j.1365-2125.2011.04005.x.

 5. Rockowitz J, et al. Bacterial meningitis. Practical guidelines for management. Drugs. 1995 Nov;50(5):838-53. doi: 10.2165/00003495-199550050-00005.

 6. Gudnason T, et al. Penetration of ceftriaxone into the middle ear fluid of children. Pediatr Infect Dis J. 1998 Mar;17(3):258-60. doi: 10.1097/00006454-199803000-00022.

 7. Schleibinger M, et al. Protein binding characteristics and pharmacokinetics of ceftriaxone in intensive care unit patients. Br J Clin Pharmacol. 2015 Sep;80(3):525-33. doi: 10.1111/bcp.12636.

bottom of page