Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Benjamin L, MD
10 Machi 2025, 15:29:12

Je, unasisimuaje G spoti?

G-spot ni sehemu ya tishu zinazozunguka tezi za mrija wa mkojo wa urethra na kisimi. Inaaminika na watafiti wengi kuwa G-spot inaweza kuwa sehemu ya mwendelezo wa kisimi kwa ndani, ambayo inajulikana kuwa na mtandao mkubwa wa mishipa ya fahamu. Baadhi ya wanawake wanaripoti kuwa eneo hili likisuguliwa hujaa damu na kupata ute mwingi zaidi.
Namna ya kusisimua g spoti
Unaweza kusisimua G spoti kwa kutumia vidole, uume au vichezeo/midoli ya kingono. Njia bora ya kusisimua G spoti ni:
Mwanamke awe ametulia – Mwili ukiwa katika hali ya utulivu, hisia za msisimko zinaweza kuwa rahisi kuamshwa G spoti inaposhikwa.
Kutumia kidole – Mtu anaweza kutumia kidole (haswa kidole cha shahada) na kukipinda kwa namna ya ishara ya "njoo" kuelekea kwenye ukuta wa juu ya uke.
Kusisimua taratibu – Kubonyeza au kupapasa eneo hili taratibu kunaweza kusababisha hisia za kufurahia au hamu ya kukojoa.
Mitindo ya ngono inayosaidia – Baadhi ya mitindo ya ngono kama vile " Staili ya ngono ya mbwa" au mwanamke kuwa juu zinaweza kusaidia kusisimua G-spot kwa urahisi zaidi.
Je, ni eneo gani la kusisimua G spoti?
G-spot inapatikana kwenye ukuta wa juu ya uke, karibu na mrija wa mkojo wa urethra(kama inavyoonekana kweenye picha), takribani inchi 1 hadi 3 (sentimita 2.5 hadi 7.5) ndani ya uke. Eneo hili linapoguswa au kusisimuliwa linaweza kusababisha msisimko mkubwa wa kingono na hata mwanamke kupata mshindo.
Faida za Kusisimua G-Spot
Kuongeza raha ya kingono – Kusisimua eneo hili kunaweza kuongeza kiwango cha msisimko wa kingono.
Kuimarisha mshindo – Baadhi ya wanawake wanapata mshindo mkali zaidi kwa kupitia msisimko wa G-spot.
Kuboresha maisha ya kingono – Wanandoa wanaweza kutumia maarifa haya kuboresha uhusiano wao wa kimapenzi.
Majina mengine ya makala hii
Makala hii pia inafahamika kwa majina yafuatayo ambayo yamejibu maswali yaliyooroshwa hapa chini:
Namna ya kusisimua G spoti
Faida za kusisimua G spoti
mapozi ya kingono ya kusisimua G spoti
Je, ni eneo gani la kusisimua G spoti?
Wapi tuapata maelezo zaidi kuhusu G spoti?
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu G spoti katika makala zifuatazo
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
10 Machi 2025, 15:35:50
Rejea za mada hii
Vieira-Baptista P, Lima-Silva J, Preti M, Xavier J, Vendeira P, Stockdale CK. G-spot: Fact or Fiction?: A Systematic Review. Sex Med. 2021 Oct;9(5):100435. doi: 10.1016/j.esxm.2021.100435. Epub 2021 Sep 9. PMID: 34509752; PMCID: PMC8498956.
Ostrzenski A. G-Spot Anatomy and its Clinical Significance: A Systematic Review. Clin Anat. 2019 Nov;32(8):1094-1101. doi: 10.1002/ca.23457. Epub 2019 Sep 8. PMID: 31464000.
Pan S, Leung C, Shah J, Kilchevsky A. Clinical anatomy of the G-spot. Clin Anat. 2015 Apr;28(3):363-7. doi: 10.1002/ca.22523. Epub 2015 Mar 4. PMID: 25740385.