top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

Maumivu ya mgongo

Maumivu ya mgongo ni tatizo linalofahamika sana kutokana na kuwapata watu wengi, watu wane walishawahi pata maumivu ya mgongo kati ya watu watano. Mara nyingi watu hawa wanaopata maumivu ya mgongo, hakuna kisababishi kinachoeleweka kusababisha maumivu hayo.

 

Mambo ambayo ni vihatarishi vya kupata maumivu ya mgongo ambayo ni;

 • Kazi za kukaa muda mrefu

 • Aina ya Maisha mtu anayoishi

 • Uzito kupita kiasi(obezit)

 • Mazoezi makali kama mpira wa miguu na mazoezi ya jimunastiki.

 • Wanawake ambao walishawahi kuwa na ujauzito

 • Uvutaji wa sigara

 • kufanya kazi za kunyanyua vitu vizito mara kwa mara

Kwa namna nyingine maumivu ya mgongo yanaweza kumaanisha dalili ya kusambaa kwa saratani mgongoni.

 

Maumivu ya mgongo yanaweza kusababishwa pia na matatizo katika uti wa mgongo  mfano;

 • Mgandamizo wa uti wa mgongo,

 • Madhaifu ya misuri ya mgongo

 • Kutumika sana kwa mgongo

 • Mgandamizo kwenye mishipa ya fahamu

 • Kupasuka kwa diski ya intavetebro

 • Kuhama kwa diski ya intavetebro

 • Athraitis ya mifupa ya uti wa mgongo

 • Kuvunjika kwa mifupa ya uti wa mgongo

 • Saratani iliyosambaa mgongoni

Sababu nje ya kwenye uti wa mgongo zinazosababisha maumivu ya mgango huwa pamoja na

 

 • Kuwa kwenye Hedhi au kipindi kabla ya kuanza kuona hedhi

 • Sisti ya ovari

 • Saratani ya ovari

 • Endometriosisi 

 • N.k

Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa 11.03.2020

Soma zaidi kuhusu matibabu ya maumivu wa mgongo kwa kubonyeza hapa

Rejea

 1. ULY CLINIC

 2. Chou R. Subacute and chronic low back pain: Nonsurgical interventional treatment. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa Juni 25, 2019.

 3. Medical problems in dentistry na crispian scully chapisho la 6

 4. Back pain. National Institute of Arthritis and Musculoskeletal and Skin Diseases. https://www.niams.nih.gov/health-topics/back-pain. Imechukuliwa Juni 25, 2019.

 5. Low back pain fact sheet. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/Patient-Caregiver-Education/Fact-Sheets/Low-Back-Pain-Fact-Sheet. Imechukuliwa Juni 25, 2019.

 6. Knight CL, et al. Treatment of acute low back pain. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa Juni 25, 2019.

 7. Low back pain. American Academy of Orthopaedic Surgeons. https://orthoinfo.aaos.org/en/diseases--conditions/low-back-pain/.  Imechukuliwa Juni 25, 2019.

bottom of page