Matibabu ya nyumbani kwa miguu inayovimba
​
Matibabu yafuatayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote akiwa nyumbani endapo ana tatizo la miguu kuvimba. Matibabu haya yanaweza kutumiwa tu endapo umeongea na daktari wako kwamba yapi ni yapi yanakufaa Zaidi kulingana na hali yako.
​
Mjongeo
Ukijongesha misuli kwenye maeneo ambayo yana uvimbe, mfano uvimbe kwenye kiwiko cha mguu au kwenye goti unatakiwa jongesha misuli ya miguu. Kufanyisha mazoezi miguu kwa kutembea mwendo au kukunja na kunyoosha kwa muda wa dakika 15 hadi 30 kunaweza saidia kupunguza uvimbe.
​
Kunyanyua miguu juu dhidi ya mwili
Hakikisha unanyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo mara kwa mara, unaweza kufanya hivi ukiwa umelala wakati wa mchana au usiku. Kuwezesha kunyanyua miguu juu, wakati umelala weka mto chini ya miguu ili miguu iwe juu Zaidi ya mwili.
​
Kukanda miguu
Kanda kwa kukamua miguu kuelekea juu kwenye magoti, tumia nguvu kidogo isipite kiasi, hii inasaidia kusukuma maji na damu yaliyozidi kuelekea kwenye.
​
Mgandamizo kwenye miguu
Unaweza tumia soksi maalumu za kugandamiza miguu yako .Soksi hizi husaidia miguu isiendelee kuvimba Zaidi na pia inapunguza uvimbe. Daktari wako atashauri matumizi ya hizi soksi na namna unavyowezazipata.
​
Kinga miguu na majeraha
Hakikisha eneo la miguu yako limekuwa safi na halijakauka, na usiliweke katika mazingira ya kupata jeraha. Ngozi ikikauka au kupata majeraha ni rahisi kupata maambukizi. Siku zote yalinde maeneo yaliyovimba kwa kuvaa vituvya kukinga kupata majeraha.
​
Punguza kiwango cha chumvi
Fuata ushauri wa dakiktari kuhusu kiwango cha chumvi unachotakiwa kutumia. Chumvi huwa na tabia ya kuhifadhi maji kwenye mwili, hivyo ukila nyingi inaweza kusababisha hali ya kuvimba ikawa mbaya Zaidi.
​
Imeboreshwa 5.11.2019