top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Miguu kuvimba, nini husababisha?

 

Miguu kuvimba husababishwa na kutuama kwa maji kwenye chembe hai za miguu, huweza kusababishwa na matatizo katika mfumo wa mishipa ya damu, mirija ya mitoki au tatizo katika figo. Unaweza kuvimba miguu kwa sababu pia ya kukaa ama kusimama mda mrefu sehemu moja.

 

Mambo yanayohusiana na miguu kuvimba ni kama;

 

1.Miguu kuvimba kutokana na kukusanyika kwa maji huweza sababishwa na

 

 • Kufeli ghafla kufanya kazi kwa figo

 • Magonjwa ya kuta za moyo

 • Kufeli sugu kufanya kazi kwa figo

 • Kufanyika makovu kwenye ini

 • DVT

 • Kufeli kwa moyo

 • Matibabu ya dawa za homoni

 • Kuziba kwa mishipa ya ngiri

 • Kuharibika kwa mishipa midogo ya ndani ya figo

 • Dawa za kutuliza maumivu kama ibrupofen na naproxen

 • Michomo kwenye kuta za moyo

 • Ujauzito

 • Madawa kama madawa ya kisukari na shinikizo la damu

 • Kusimama kwa mda mrefu, kukaa kwa mda mrefu kama kwenye ndege na gari

 • Magonjwa ya mishipa ya damu

 • Mishipa ya damu ya vein kushindwa kurudisha damu kwenye moyo

 

2.Miguu kuvimba kutokana na michomo ndani ya chembe hai za miguu huweza kusababishwa na

 • Kuvunjika kwa mfupa

 • Maambukizi kwenye ngozi

 • Gauti

 • Maambukizi kwenye vidonda vya miguuni

 • Maambukizi kwenye vijifuko vya maji katika maungio ya miguu

 • Misuguano ya mifupa katika maungio

 • Baridi yabisi

 • Jeraha kwenye maungio ya visigino

bottom of page