top of page

Mlo wa siku

Nguvu za kiume 2

Mkusanyiko wa sumu mwilini zinazochangiauharibifu katika mishipa ya damu huweza kupunguzwa na matumizi ya sharubati za matunda mbalimbali na hivyo kuimarisha ufanyaji wa tendo la ndoa.

Sharubati kwa afya ya tezi dume

Sharubati hii ya kiafya inayotengenezwa kwa komamanga, tikiti maji, soya, na mbegu za kitani ni chanzo bora cha virutubishi na viuajisumu. Husaidia kuboresha afya ya moyo, kinga ya mwili, na mmeng’enyo wa chakula.

Sharubati ya Papai na nanasi: Kukata kitambi

Sharubati hii ya papai, nanasi, na chai ya hibiscus husaidia kupunguza fumbatio na kuboresha afya ya utumbo. Inasaidia pia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, lakini inapaswa kuepukwa na watu wenye matatizo maalum ya kiafya.

Sharubati ya brokoli: Kinga ya saratani ya matiti

Sharubati kinga ya matiti ikitumika mara nne kwa siku kabla ya kifungua kinywa, baada ya chakula cha mchana, alasiri, na kabla ya kulala hutoa kinga bora dhidi ya saratani ya matiti. Inajumuisha viinilishe na viuajisumu kutoka kwenye brokoli, stroberi, na maziwa ya soya.

Tiba ya kuchelewesha uzee

Mkusanyiko wa sumu mwilini zinazochangia uzee wa haraka huweza kupunguzwa na matumizi ya sharubati za matunda mbalimbali na hivyo hivyo kuchelewesha uzee. Matumizi ya muda mrefu huwa na manufaa zaidi.

bottom of page