top of page

Dalili za mtoto kucheza tumboni ni zipi?

Updated: Jul 11, 2023


Dalili za mtoto kucheza Tumboni

Mjamzito huanza kuhisi mtoto akicheza tumboni kuanzia wiki ya 16 hadi 20, hata hivyo baadhi ya wanawake huwahi au kuchelewa kuhisi tofauti na wiki hizi.

Dalili za kucheza kwa mtoto tumboni huweza kuchanganywa na mijongeo mbalimbali katika tumbo hivyo wajawazito wengi hushindwa kutambua katika wiki za mwanzo za ujauzito.

Kucheza kwa mtoto tumboni ni ishara muhimu inayoonesha kuwa mtoto yu hai na mwenye afya njema.


Dalili za mtoto kucheza tumboni

Wajawazito hueleza kuwa hisia za mtoto kucheza tumboni huweza kuelezewa kwa namna zifuatazo;

  • Mjongeo mithili ya kuogelea kwa kitu tumboni

  • Mijongeo mithili ya kutembea kwa kitu tumboni

  • Mijongeo mithili ya mpwito

  • Mijongeo mithili ya mdundo

  • Mijongeo halisi ya miguu na mikono ya mtoto katika hatua za mwisho za ujauzito


Nini unapaswa kufahamu zaidi kuhusu dalili za mtoto kucheza tumboni?

Kucheza kwa mtoto tumboni ni ishara muhimu inayoonesha kuwa mtoto yu hai na mwenye afya njema.


Endapo hauhisi mijengeo ya mtoto au imepungua kasi fika katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi zaidi.


Rejea za mada

  1. Fetal Movement – When You feel Baby kick.webmd.com. https://www.webmd.com/baby/fetal-movement-feeling-baby-kick. imechukuliwa 03.07.2023

  2. How does it feel when a baby moves during pregnancy? Medical news today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/what-does-it-feel-like-when-baby-moves. imechukuliwa 03.07.2023

  3. Common Pregnancy Complaintsand Questions. Medscapehttps://emedicine.medscape.com/article/259724-overview#a1. imechukuliwa 03.07.2023

2,716 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page