top of page

Dawa ni sumu kwenye ujauzito

Matumizi ya dawa wakati wa ujauzito


Ni nini mama mjamzito unatakiwa fahamu kuhusu dawa?


Dawa zinaweza kuleta madhara hasi kwa kijusi au mtoto kwenye kipindi chochote kabla au baada ya kupata ujauzito na baada ya mtoto kuzaliwa. Ni muhimu kuweka akilini kuwa kutumia dawa kwenye umri wa uzazi kwa mwanaume au mwanamke inaweza kuambatana na madhara kwa mtoto.


Madhara ya dawa kipindi cha kwanza cha ujauzito

Katika kipindi cha kwanza cha ujauzito,wiki kumi na mbili za mwanzoni, ni kipindi ambacho uumbaji wa viungo mbalimbali vya mtoto unatokea. Matumizi ya dawa kipindi hiki huweza pelekea madhaifu ya kiumbaji kwa kijusi au mtoto tumboni mfano kukosewa kwa uumbaji wa ubongo, moyo, mifupa, mishipa ya fahamu n.k

Dawa nyingi zinafahamika kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kipindi hiki mfano diethylstilbestrol ambayo ilikuwa inatumika zamani kuzuia mimba kutoka na zingine.


Wazazi wanapaswa kufahamu kuhusu dawa yoyote ile wananayotarajia kutumia kama inamadhara kipindi hiki hata kabla ya kupata ujauzito.


Madhara ya dawa kipindi cha pili na tatu cha ujauzito


Wakati wa kipindi cha pili na tatucha ujauzito, uumbaji wa viungo mbalimbali vya mtoto unakuwa umekamilika, kinachofuata ni ukuajiwa kikazi na kiumbo wa viungo mbalimbali. Endapo utatumia dawa zinazozuia maendeleo haya kuendelea ktokea katika asili yake, unaleta madhaifu au sumu kwenye viungo hivyo.


Dawa zinazotolewa muda mfupi kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua, huweza kuwa na madhara kwenye uchungu na kichanga baada ya kuzaliwa.


Ikumbukwe pia kuwa, si kila madhara ya uharibifu wa dawa huonekana baada ya kuzaliwa, madhaifu mengine huonekana miezi au miaka kadhaa baada ya kuzaliwa. Mfano wa madhara ya baadaye ni saratani ya adenosakoma ya uke inayotokea kwa watoto ambao mama alitumia dawa ya diethylstilbestrol wakati wa ujauzito wake, madhara ya kiakili au ukuaji na kijamii huweza tokea pia.


ULY CLINIC imejaribu kuandika dawa ambazo zinaweza kuwa na madhara kwenye ujauzito, ikiwa imeonyesha ni kwenye kipindi gani cha ujauzito dawa hizo zinaleta shida, na dawa gani ambazo zina madhara makubwa kwenye ujauzito ili kuepukwa.

Taarifa zilizoandikwa kwenye tovuti ya ULY CLINIC zinatokana na tafiti au matokeo ya matumizi ya dawa kwa binadamu wajawazito. Taarifa kutoka kwa wanyama waliopewa dawa hizo zipo pia kwa dawa ambazo hazijatumika kwa mama mjamzito au endapo hakuna taarifa kutoka kwa binadamu wajawazito.


Dozi ya dawa kwa wajawazito inaweza takiwa kufanyiwa marekebisho kwa sababu ya mabadiliko ya kifiziolojia yanayotokea wakati wa ujauzito.


Hitimisho muhimu kuhusu dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi ya dawa kwenye ujauzito yafanyike tu endapo faida kwa mama ni kubwa kuliko hatari kwa kijusi na mtoto tumboni, dawa zozote zinatakiwa kuepukwa kipindi cha kwanza cha ujauzito kama itawezekana.


Dawa ambazo zimeshawahi kutumika kwenye ujauzito na kuonekana kuwa salama zinatakiwa tumika kama mbadala wa dawa mpya ambazo hazina taarifa za usalama wake kutoka kwenye tafiti, hata hivyo dozi ndogo zaidi yenye uwezo wa kufanya kazi inatakiwa itumike.


Dawa chache zimethibitika kuwa ni teratojenia kwenye vipindi vyote vya ujauzito wa binadamu.


Hakuna dawa yoyote ile ambayo ipo salama kwa asilimia 100 kwenye ujauzito. Tumia dawa endapo kuna ulazima sana.


Kutokuwepo kwa taarifa ya madhara ya dawa fulani kipindi cha ujauzito haimaanishi kuwa dawa hiyo ni salama.


Wapi utapata taarifa zaidi kuhusu dawa na ujauzito?

Rejea za mada hii


 1. Eleni S. Tsamantioti, et al. Teratogenic Medications. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK553086/. Imechukuliwa 23.06.2021

 2. Drugs in pregnancy. www.uktis.org. Imechukuliwa 23.06.2021

 3. BNF 2018-2019, prescribing drugs in pregnancy

 4. @ulyclinic. Madhara ya dawa kipindi cha ujauzito. https://www.ulyclinic.com/madhara-ya-dawa-kwa-mjamzito-na-mto. Imechukuliwa 23.06.2021

 5. @ulyclinic. Dawa salama kipindi cha ujauzito. https://www.ulyclinic.com/dawa-salama-kipindi-cha-ujauzito. Imechukuliwa 23.06.2021

 6. Better Health Channel. Drugs, medication and birth defects. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/ConditionsAndTreatments/drugs-medication-and-birth-defects. Imechukuliwa 23.06.2021

 7. Thalidomide Teratogenic Effects Linked to Degradation of SALL4: After 60 years, researchers have now shed light on the mechanism underlying thalidomide's devastating teratogenic effects. Am J Med Genet A. 2018 Dec;176(12):2538-2539.

 8. Kennedy MLH. Medication management of bipolar disorder during the reproductive years. Ment Health Clin. 2017 Nov;7(6):255-261.

 9. Ornoy A. Neuroteratogens in man: an overview with special emphasis on the teratogenicity of antiepileptic drugs in pregnancy. Reprod Toxicol. 2006 Aug;22(2):214-26.

 10. Mantovani A, et al. Delayed developmental effects following prenatal exposure to drugs. Curr Pharm Des. 2001 Jun;7(9):859-80.

 11. Kennedy D, et al. Valproic acid use in psychiatry: issues in treating women of reproductive age. J Psychiatry Neurosci. 1998 Sep;23(4):223-8.

 12. Ornoy A. Valproic acid in pregnancy: how much are we endangering the embryo and fetus? Reprod Toxicol. 2009 Jul;28(1):1-10.

 13. Nie Q, Su B, et al. Neurological teratogenic effects of antiepileptic drugs during pregnancy. Exp Ther Med. 2016 Oct;12(4):2400-2404.

 14. Katarina Dathe, et al. The Use of Medication in Pregnancy. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6935972/. Imechukuliwa 23.06.2021
125 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentários


bottom of page