top of page

Unapataje mtoto kwa wakati? | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Kama kupata mimba imekuwa ni changamoto kwako na mpenzi wako, basi jua kuwa hauko peke yako na tatizo hili. Asilimia kumi hadi 15 ya wanandoa nchini Tanzania ni wagumba (tasa). Utasa huelezewa kuwa ni tatizo la  kutokuwa na uwezo wa kupata mimba licha ya kuwa unashiriki tendo la ndoa pasipo kutumia kinga au njia za uzazi wa mpango angalau kwa mwaka mmoja au baada ya miezi sita kwa baadhi ya watu.

Utasa unaweza kusababishwa na sababu moja ama nyingi zilizo kati yako wewe na mpenzi wako, au mchanganyiko wa mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuzuia mimba kutungwa au kuendelea. Kwa bahati nzuri, kuna matibabu  mengi ya usalama, ufanisi na  Msingi kwa ajili ya kukabiliana utasa-ugumba. Matibabu haya kwa kiasi kikubwa huboresha ama kurudisha nafasi yako ya kuwa mjamzito


Dalili za Ugumba-Utasa

Wapenzi wengi walio wagumba, hupata mimba ndani ya miezi sita ya kwanza ya kujaribu kutafuta mimba baada yha ushauri kutoka kwa daktari. Kwa ujumla, baada ya miezi 12 ya kujamiiana  mara kwa mara bila kinga, asilimia 90 yawanandoa hupata mimba. Wengi wa wanandoa wenye ugumba huweza kupata mimba bila matibabu yoyote

Ishara kuu ya utasa ni kukosa uwezo kwa wanandoa kupata mimba. 

Mara nyingi hakuna dalili za wazi ama za kuonekana zinazomsema mtu kuwa anaugumba

35 views0 comments

Recent Posts

See All

Commentaires


bottom of page