top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Darasa la kisukari | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Watu wengi walio na ugonjwa wa kisukari walianza kupata dalili lakini hawakuwa wanajua mpaka ugonjwa ulipoanza kuonyesha madhara, Kisukari aina ya 2 huzuilika endapo mtu mwenye vihatarishi ataepukana navyo kwa kupewa uelewa zaidi kuhusu namna ugonjwa unavyoweza kutokea na kuzuilika. Inafahamika Madhara yanayotokana na kisukari huweza kukingwa ili yasitokeee, na ni rahisi pia kukinga madhara makubwa yanayoweza kutokea endapo utadhibiti kiwango cha sukari


Ni vema kujua namna gani unaweza kudhibiti tatizo la kisukari ili uishi maisha bora sawa na wengine. Na pia endapo hauna kisukari ni vema ukajua pia mbinu gani unaweza kutumia kujikinga na ugonjwa wa kisukari.


Nitakuwa na darasa siku ya Jumamosi kuanzia sa 10 jioni katika Ukumbi wa #cedha arusha ili kutoa elimu kwa wagonjwa wa #kisukari kuhusu Namna ya kuishi na kujikinga na kisukari. Elimu hii ni bure kabisa. Tutapanga kwa pamoja namnaya kutengeneza milo na kupanga mazoezi. Hii ikiwa na madhumini ya kudhibiti na kujikinga na kisukari pamoja na madhara yanayoweza kutokea kwenye moyo, mishipa ya damu na fahamu n.k

Nawakaribisha sana watu wote.

Vitu vingine unavyoweza kunufaika navyo ni;


  • Kupimwa sukari

  • Kupata vitabu vya kisukari

  • Kupimwa macho na masikio

  • Kupima shinikizo la damu

Nawakaribisha nyote


Kwa mawasiliano tumia namba zilizo chini ya tovuti hii

107 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page